Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake wanachama Saccos wafundwa kukabili athari mikopo umiza

Fedhapic Wanawake wanachama Saccos wafundwa kukabili athari mikopo umiza

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya wanawake 250 wanachama wa vyama vya Kuweka na Kukopa (Saccos) nchini wamenolewa kuhusu afya ya akili kuwawezesha kukabiliana na msongo wa mawazo unaotokana na mikopo ya mitaani.

Pamoja elimu ya afya ya akili, wanawake hao kutoka mikoa mbalimbali nchini pia wamenolewa kuhusu elimu ya fedha na maendeleo binafsi, lengo likiwa ni kuwapa mbinu za kutumia vema mikopo kwa maendeleo na ustawi kiuchumi.

Akizungumza jijini Mwanza wakati wa Jukwaa la Wanawake wa Saccos linaloambatana na maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika jijini humo, Mratibu wa jukwaa hilo, Leah Daudi amesema wanawake ni miongoni mwa makundi ya kijamii inayopata msongo wa mawazo kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo mikopo umiza mitaani.

“Tunaamini maafunzo haya yatawapa mbinu namna ya kupunguza athari ya msongo ya mawazo unaotokana na majukumu mengi ya kijamii na kiuchumi inayowakabili wanawake,’’ amesema Leah

Akizungumzia mikopo na maendeleo, kiongozi huyo wa jukwaa la wanawake wa saccos amesema kuna muelekeo kuwa wanawake wengi hawana maendeleo binafsi licha ya kuchukua mikopo kutoka kwenye saccos zao au taasisi zingine za fedha; hali inayohitaji kupatiwa ufumbuzi.

‘’Wanawake wanaonekana wapambanaji kiuchumi lakini ukiwaangalia hawana maendeleo binafsi, tumeona ni vema kuwapa elimu ya fedha kuwawezesha kutumia vema mikopo wanachukua kwa ajili ya mitaji ya biashara na ujasiriamali,’’ amesema Leah

kwahiyo tumeweza kuwakutanisha na wawezeshaji mbalimbali ili wajifunze,”amesem Leah

Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake viongozi wa Saccos, Somoe Nguhwe amewataka wananwake kuongeza mwamko na muitikio katika shuguli mbalimbali za kijamii na kiuchumi kumaliza tatizo mfumo dume.

‘’Wanawake tuondokane na tatizo la kutojiamini kuhusu uwezo wa kuongoza; tujitokeze kwa wingi kugombea nafasi za uongozi kila fursa zinapojitokeza kudhihirisha uwezo wetu katika masuala ya kijamii na kiuchumi,’’ amesema Somoe

Amesema ili kufanikisha lengo hilo, jukwaa hilo limeanzisha mitandao ya wanawake ya kikanda kuwahamasisha wanawake wanachama wa Saccos kuchangamkia furasa za uongozi kwenye vyama vyao.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi amewahakikishia wanawake wanachama wa Saccos kuwa Serikali itaendelea kuweka na kuimarisha mifumo itakayowawezesha wanawake na makundi maalumu ya kijamii kufikia na kunufaika na fursa za kiuchumi kwenye maeneo yao.

Kwa mujibu wa Naibu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika na Udhibiti kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini, Collins Nyakunga, wanawake 698,476 ni kati ya wanachama zaidi ya milioni 1.8 kwenye saccos 759 zilizsajiliwa nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live