Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake kuwekewa mazingira wezeshi ya ufanyaji biashara mipakani

74443 Manyanya+pic

Thu, 5 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya amesema Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kuhakikisha uwepo wa mazingira wezeshi ya wafanyabiashara wanawake wanaofanya biashara zao mipakani.

Amesema mwanamke ni nguzo ya mabadiliko kiuchumi hivyo mazingira wezeshi yatasaidia kukuza biashara zao ili kuleta mchango katika kukuza pato la Taifa.

Manyanya ameyasema hayo leo Alhamisi Septemba 5, 2019 wakati wa ufunguzi wa kongamano la wanawake wafanyabiashara mipakani, lililoandaliwa na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake (UN Women) kwa ajili ya kujadili changamoto na mafanikio ya wanawake wafanyabiashara mipakani.

Amesema Serikali inatambua mchango wa mwanamke, itaendelea kutoa elimu za biashara, mafunzo mbalimbali ili waweze kufanya biashara zenye viwango katika soko la ndani na nje.

"Hakuna asiyejua kuwa mwanamke ni chachu ya maendeleo, hivyo hakikisheni mnatumia fursa ya kongamano hili kubadilishana uzoefu  kutoka nchi jirani ya Uganda, hakikisheni mchango wenu na mawazo yenu leo yanakuwa na manufaa katika biashara zenu kwa ajili ya taifa letu,” amesema.

 

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz