Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake kuendelea kupewa kipaumbele majukuwaa ya biashara

WhatsApp Image 2023 11 20 At 10.jpeg Wanawake kuendelea kupewa kipaumbele majukuwaa ya biashara

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanawake Wafanyabiashara na Wajasiriamali wameendelea kupewa kipaumbele kwenye majukwaa mbalimbali ya biashara na ujasiriamali ili kuhakikisha wanapata maendeleo na kukua kiuchumi kupitia shughuli hizo za biashara na ujasiriamali.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila kwenye Kongamano la Maandalizi na Masoko kwa Wanawake na Vijana Wajasiriamali lililofanyika jijini Dar es Salaam.

Mhe. Chalamila amesema taifa la Tanzania limeendelea kuandaa na kuratibu sera mbalimbali za kuwawezesha Wanawake na Vijana wanafurahi na kupata maendeleo kupitia biashara hizo.

“Dar es Salaam tumekuwa na kipaumbele kikubwa kutoa fursa za biashara kwa wanawake ili kuwafanya kukua na kupata maendeleo kupitia biashara hizo na ujasiriamali,” amesema Mhe. Chalamila

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Women Chember of Commerce (TWCC), Mwajuma Hamza alisema wanatoa mafunzo hayo kwa Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wanawake katika majukwaa makubwa ili Kuwawezesha kuyafikia na kupata mafanikio ili kukua kiuchumi na kupata maendeleo.

“Wanawake hajalala wanaendelea kuchangamkia fursa zaidi kwenye majukwaa mbalimbali ili kufikisha biashara zao ili zikue, sisi TWCC tunaendelea kuhamasisha zaidi hata wale Wanawake Wafanyabiashara wa mikoani ili na wao wachangamkie fursa hizi zilizopo,” amesema Mwajuma.

Vile vile, baadhi ya Wanawake Wafanyabiashara na Wajasiriamali mbalimbali wameshukuru TWCC kuwapa mafunzo hayo kupitia Kongamano hilo la Wanawake na Vijana hususani kushiriki kwneye majukwaa makubwa ya fursa za biashara ili kupeleka biashara hizo na kukua kimaendeleo na kukua kiuchumi kiujumla.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live