Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Wanawake changamkieni fursa kwenye ubaharia’

BAHARIA TAALUMA ‘Wanawake changamkieni fursa kwenye ubaharia’

Mon, 26 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TAKWIMU zinaonesha idadi ya mabaharia Tanzania ni takribani 9,000, huku wanawake wakiwa ni chini ya asilimia moja.

Takwimu hizo zimetolewa na Mkuu wa Wilaya Ilemela (DC), Hassan Masala, wakati akifunga maadhimisho ya siku ya mabaharia duniani leo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, yaliyoratibiwa na Shirika la Uwakala wa Meli nchini (TASAC).

Kutokana na hali hiyo, akawashauri vijana wa kike kujikita katika masomo ya ubaharia, si tu kuziba pengo la ubaharia kijinsia, bali kuchangamkia fursa zilizomo katika sekta ya uchukuzi kwa njia ya maji.

Amesistiza kwamba sekta ya uchukuzi kwa njia ya maji ina fursa nyingi kiuchumi, kwani asilimia 90 ya biashara yote ya kimataifa duniani inabebwa na meli.

“Kwa hiyo mabaharia ndio nguzo muhimu katika kukuza uchumi wa dunia na taifa kwa ujumla, kwani ndio wanaohusika kusafirisha biashara hizo,” amesema na kuongeza kuwa:

“Wakati huo huo mabaharia ni kiungo muhimu katika kulinda mazingira kwenye maji, kama mikataba ya kimataifa iliyosainiwa na serikali ya Tanzania inavyoelekeza, ili kulinda afya za viumbe waliomo na watumiaji wa usafiri huo.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live