Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaouza sukari bei kubwa wakamatwa

Sukari Zanzibar Wanaouza sukari bei kubwa wakamatwa

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amewahakikishia Watanzania kuwa hadi kufikia February 15,2024 hali ya utulivu ya upatikanaji wa sukari itakuwepo huku akisisitiza kwamba bei elekezi ya sukari ni Tsh. 2700 hadi 3200 na tayari Wafanyabiashara wanaouza sukari bei ya juu wameanza kukamatwa.

Bashe amesema hayo leo wakati akiongea na Wakazi wa Arusha kwa njia ya simu baada ya kupigiwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Paul Makonda ambaye yupo ziarani Mkoani humo na akamtaka aelezee hali ya halisi ya sukari Nchini na sababu za bei kupanda.

Bashe amenukuliwa akisema “Nataka niwaombe Wananchi watulie na niwahakikishie kwamba Serikali imechukua hatua na niwaombe radhi kwa taharuki iliyojitokeza kutokana na viwanda vyetu kuathirika kwenye uzalishaji tumeamua kuagiza sukari kutoka nje na shehena ya kwanza inaanza kuingia kuanza January 26 hadi 30, 2024 na tumetoa vibali vya jumla ya tani zaidi ya laki moja”

“Nataka niwaambie Watanzania wote kupitia mkutano wako kwamba mpaka February 15,2024 hali ya utulivu ya upatikanaji wa sukar na sio kwamba Nchini hakuna sukari bali kuna tabia ya Wafanyabiashara ambao tumekuwa tukiwalinda kwa muda mrefu kutengeneza upungufu usio halali, tumewakamata Watu wote ambao wanauza sukari zaidi ya bei elekezi na bei elekezi ya Serikali bei ya sukari haitotakiwa kuzidi kati ya Tsh. 2700 mpaka Tsh. 3200 kwa Nchi nzima “

Chanzo: www.tanzaniaweb.live