Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaouza nyama zisizo na mihuri wafikiwa

Nyama Mihuri (600 X 420) Wanaouza nyama zisizo na mihuri wafikiwa

Wed, 18 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi nchini kupitia Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo limewataka wafanyabiashara wa kuuza nyama kuhakikisha wanauza nyama ambazo zimegongwa mihuri kutoka mamlaka zinazohusika.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP. Simon Pasua wakati alipotembelea mabucha ya kuuza nyama katika Soko Kuu la Arusha.

ACP. Pasua amewataka wauza nyama wote kuhakikisha wanafuata kanuni na taratibu zinazowaongoza sambamba na kuuza nyama ambazo zinatoka katika machinjio ya Serikali ambapo mifugo inapimwa kabla ya kuchinjwa.

Mkuu wa Soko hilo Bwana Datus Renatus mbali na kupongeza jeshi la Polisi, amesema wamejifunza mambo mengi kupitia maelekezo mbalimbali ambayo wameyapata ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara wa nyama kuhakikisha wanafuata kanuni na taratibu za biashara zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live