Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wasusia fidia ya Acacia

44907 Caccpic Wananchi wasusia fidia ya Acacia

Tue, 5 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tarime. Wakazi 203 wa vijiji vinne vinavyozunguka mgodi wa Acacia North Mara wamesusia fidia iliyotolewa na mgodi huo kwa madai kuwa fedha wanazolipwa ni kidogo.

Mkuu wa wilaya ya Tarime Charles Kabeho, amesema leo Jumanne Machi 5, 2019 kuwa wananchi hao wamesusa kuchukua fidia hiyo wakidai fedha wanazolipwa hazilingani na thamani halisi ya ardhi na mazao yao.

"Mwitikio ni mdogo, wengi walijitokeza walipoona kiasi kilichoandikwa kwenye cheki zao hawakuridhika na kuamua kuacha kuchukua," amesema Kabeho.

Katika shughuli hiyo ililoanza jana Jumatatu mgodi huo ulitenga zaidi ya Sh3.8 bilioni kwa ajili ya kulipa fidia kwa vijiji vya Mjini kati, Nyakunguru, Nyamichele  na  Nyangoto.

Mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Malima amesema baada ya kutoa taarifa hiyo kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mara pamoja na Waziri wa Madini Doto Biteko wameamua kwenda  Nyamongo ili kujua tatizo ni nini.

Endelea  kufuatilia Mwananchi kujua kitakachojiri



Chanzo: mwananchi.co.tz