Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi waomba kupatiwa maeneo ya kulima

Kilimo House Wananchi waomba kupatiwa maeneo ya kulima

Mon, 20 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WANANCHI wa kijiji cha Kagera Nkanda, Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wameiomba serikali kuwapatia maeneo kwa ajili ya kilimo ili kuondokana na changamoto ya kuingia kwenye maeneo ya hifadhi au kukodi maeneo kwa ajili ya kilimo kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya Kasulu kwa gharama kubwa.

Wananchi hao wametoa kilio hicho mbele ya kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe aliyekuwa akifanya mkutano wa hadhara ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembelea na kufanya mikutano katika majimbo manane mkoani Kigoma ambapo wananchi wamesema kuwa kijiji chao kina tatizo kubwa la ukosefu wa maeneo kwa ajili ya kilimo jambo linaloathiri maisha yao kiuchumi.

Desai Gabriel Kasogota mmoja wa wananchi wa kijiji cha Kagera Nkanda wilayani Kasulu alisema kuwa walipiga kelele kuomba kuongezewa maeneo na serikali iliwaongezea hekari 10,000 lakini wameshangaa Halmashauri ya Wilaya Kasulu imechukua eneo hilo na kuwakodisha wananchi ambao wanalazimika kulipa 50,000 kwa hekari moja kwa msimu.

Mkazi mwingine wa kijiji hicho, Isac Mbonankuze alieleza serikali imeshindwa kusimamia kikamilifu changamoto ya eneo hilo na kuimaliza badala yake viongozi wamekuwa wakijinufaisha kwa namna mbalimbali ikiwemo masuala ya kisiasa kama sehemu ya kujipatia kura lakini pia wengine wanatumia eneo hilo kwa faida yao kiuchumi.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara kwenye kijiji hicho Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amemtaka Waziri wa ardhi, Waziri wa maliasili na utalii na Waziri wa TAMISEMI kulifanyia kazi suala hilo ili kuondoa kero hiyo inayosababishwa na watendaji wa serikali katika eneo hilo ambao wamekuwa wakisababisha migogoro na kujinufaisha na kuwepo kwa migogoro hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live