Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi waomba elimu matumizi ya vifurushi

Elimu Vifurushi Wananchi waomba elimu matumizi ya vifurushi

Wed, 11 May 2022 Chanzo: eatv.tv

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam bado wameonesha kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu makato na bei za vifurushi ambavyo hutolewa na watoa Huduma za mawasiliano hivyo kuiomba mamlaka ya mawasiliano nchini kuzidi kutoa elimu hii kwa Watanzania.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA imeonyesha zaidi ya asilimia 95 ya watumiaji wa huduma za mawasiliano hupendelea kutumia Huduma za vifurushi kwa kuwa zinapunguzo kubwa.

Aidha zipo sababu ambazo zinatajwa kuongeza matumizi ya kifurushi ikiwemo uwezo wa simu janja,ubora wa picha na video zinazopakuliwa pamoja na mtumiaji kuwa na program rununu nyingi.

Taarifa hiyo imeonyesha kuwa kwa Tanzania bei za Huduma za data iko chini zaidi kwa MB kwa nchi za Afrika Mashariki na SADC ambapo wastani wa gharama za data nchini ni takribani Dola 0.75 za kimarekani  Kwa GB Moja ya data sawa na shilingi 1725 huku Kwa bara la Africa Tanzania ikiwa nchi ya 6 kati ya 52 zenye gharama nafuu za data.

Chanzo: eatv.tv