Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wamkumbuka Kikwete

32586 KIKWETEPIC Tanzania Web Photo

Thu, 20 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Ujumbe wa pongezi aliouandika Rais mstaafu Jakaya Kikwete kuhusu msanii, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’ kuingiza sokoni manukato yake yaitwayo FYN umeibua hisia za wananchi mtandaoni, kueleza jinsi walivyomkumbuka Rais huyo wa Awamu ya Nne.

Kikwete aliweka picha katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter akiwa ameketi na msanii huyo, huku akiandika ujumbe jinsi alivyomshauri kufanya shughuli nyingine zaidi ya muziki jambo ambalo Mwana FA amelifanya.

Mmoja wa wachangiaji katika ukurasa huo, wolperwemanation alienda mbali zaidi na kuhoji kuwa ikiwezekana waganga wanaojitangaza kuwa na uwezo wa kuwarejeshea pamoja wapenzi walioachana, basi wafanye hivyo kumrejesha Kikwete madarakani.

Katika ujumbe wake huo kwa MwanaFA, Kikwete ameandika, “Kuna siku nilimsihi MwanaFA  na wanamuziki wengine kufanya shughuli nyingine zaidi ya muziki pekee. Nimefarijika leo kunitembelea na kutambulisha bidhaa yake mpya ya ‘body spray’. Hii ni hatua kubwa na nzuri kwa vijana wetu. Tuwaungishe.”

Mchangiaji mwingine,  Goodluck Paroko ameandika kuwa Kikwete amekuwa mzazi wa wasanii wote wa Tanzania kwa kipindi kirefu hata baada ya uongozi wake.

“Kila mwenye hitaji lake na masumbuko ya moyo anakimbilia Msoga. Baraka za wazee wenye maana ni muhimu,” amesema Paroko.

Mchangiaji mwingine,  dvj25december amesema Kikwete anakumbukwa kwa mengi ikiwemo kuunga mkono juhudi za vijana, “Hayupo nyuma. Huyu ni mtu wa huruma na busara kubwa mno tumekumiss.”

Naye, Hussein Mohammed amesema, “Tumekukumbuka rais wetu kama ingewezekana tungependa kukuona unarudi katika kiti chako.”

Mwandishi Juniour  ameandika kuwa vijana wanamkumbuka Kikwete kwa hekima na busara zake katika kuwashauri vizuri na kupata mitaji ya akili fedha wakati alipokuwa rais.

“Lakini sasa hivi mitaji inaenda kufa mzee wetu biashara ngumu sana kwa sasa hata huyo sijui kama atatoboa kwenye soko hili la sasa tumekukumbuka,” amesema Juniour

Don chepe amesema vijana hawataacha kumkumbuka Kikwete kutokana na kujali kwake kwa sababu aliyekuwa na shida haikupita bila rais huyo mstaafu kutia mkono.

“Umefanya tugundue vitu vingi sana kwenye maisha yako ikiwemo ushirikiano mkubwa kwa vijana, tunakukumbuka,” amesema Don cheupe. 



Chanzo: mwananchi.co.tz