Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi waaswa kununua bidhaa za Tanzania

Wananchi Waaswa Kununua Bidhaa Za Tanzania.jpeg Wananchi waaswa kununua bidhaa za Tanzania

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika kuhakikisha Wajasiriamali wanapenya kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi Serikali kwa kushirikiana na Taasisi ya GS1 wamehamasisha wananchi kununua bidhaa zinazozalishwa nchini na nyenye msimbomilia ( Barcodes au QR code ).

Akizungumza wakati wa kufunga wiki Barcode kitaifa 2023 iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo Juni, 19. Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema kuwa 620 ni Mali ya Watanzania hivyo jamii imehamasishwa kununua mali ya Tanzania kwa 620.

"Tujisikie fahari kununua mali ya Tanzania yenye 620, ukinunua Mali ya Tanzania yenye 620 maana yake umesaidia nchi kupata mapato, pia pale unapoenda kutafuta Barcode kuna malipo unafanya hapo pia unachangia mapato ya Serikali." Amesema Mpogolo

Pia amesema kuwa Barcode ya Tanzania itapunguza maneno ya kashfa juu ya nchi kuwa inazalisha bidhaa zisizokuwa na ubora pia itapunguza bidhaa za nchi nyingine zinapoharibika na kusema ni bidhaa za Tanzania.

Akizungumzia umhimu wa Barcode amesema kuwa alama za Msimbomilia kwenye bidhaa za Tanzania Mpogolo amesema alama hizo zitasaidia Wafanyabiashara kupeleka bidhaa katika mataifa mbalimbali duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live