Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi Handeni walia bei za vyakula zikipaa

Handeni Mazao.png Wananchi Handeni walia bei za vyakula zikipaa

Fri, 15 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya bidhaa zinazotumika kuandaa futari katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwenye masoko mbalimbali zimeanza kupandishwa bei, huku wengine wakipunguza idadi wanapoziuza.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Digital kwenye masoko wilayani Handeni, leo Ijumaa Machi 15, 2024 umebaini bidhaa zilizopanda bei ni magimbi na nazim huku nyingine kama mihogo na ndizi zikiwa kimbilio la wengine kutokana na unafuu wa bei.

Fungu moja la mihogo inayopangwa mitano mpaka sita ni Sh1,000 sawa na ndizi za kawaida, bidhaa nyingine kama tambi bei zake zimebaki kama awali ambapo zipo za kupima kwa kilo na zilizofungashwa tayari.

New Content Item (1)

Mkazi wa Handeni, Semeni Chihumpu amesema bidhaa kama magimbi, wafanyabiashara hawajapandisha bei ila fungu la Sh2,000 ambalo lilikuwa na vipande vinne vikubwa, kwa sasa limepunguzwa na kuwekwa vipande vidogo vitatu ila bei ni ile ile.

"Hata viazi vitamu navyo bei yake imepanda, kwani fungu la viazi vitano ilikuwa Sh1,000 ila sasa ni Sh2,000, nazi za Sh500 kwa sasa zimepanda ni Sh800 mpaka Sh1,000 hapa Ramadhan haijafika hata wiki moja, sijui ikifika kumi la pili na tatu bei zitakuwaje," amesema Semeni.

Mfanyabishara wa ndizi katika soko kuu la Handeni, Hamida Suphiani amesema bidhaa kama ndizi, mihogo na viazi vitamu ndio bidhaa zinapatikana kwa wingi kwa wakulima na ndio sababu bei yake haipo juu.

Amesema kwa bidhaa kama nazi ndio inatumika zaidi wakati wa Ramdhani, ndio sababu bei yake inapanda.

"Magimbi yataendelea kupanda bei na hii sio mwaka huu tu, kila mwaka magimbi bei yake inakuwa juu na hii ni kutokana kwamba ni dhidaa adimu sokoni,hakuna mtu atasema anaumwa na tumbo akila gimbi hutasikia hilo, ila wengi hawapendi bidhaa kama viazi tamu wakidai vinaumiza tumbo," amesema.

Bei ya sukari nayo katika baadhi ya maduka inaonekana kupanda kutoka Sh3,600 bei elekezi ya Serikali kwa ukanda wa kaskazini na sasa inauzwa Sh4,000.

Mkazi wa Zizini wilayani Handeni, Hemedi Mhina ameshauri mamlaka za Serikali zinazohusika na kusimamia mambo ya bei kwenye masoko kupita na kuangalia kwenye maduka na katika masoko ukiukwaji wa bei hasasukari na wachukue hatua.

"Sisi wananchi ndio tunaumia na hizi bei, sukari inatumika sana kwenye futari, tunaomba wananchi wenzetu ambao ni wafanyabiashara wasitumie mwezi huu kuumiza," amesema Hemedi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live