Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi 7,208 wanufaika na Sh1.1 bilioni za Tasaf Mwanza

Tasaf Pic Data Makilagi ametoa ufafanuzi huo mapema hii leo

Tue, 17 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) kupitia Mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN II) umelipa Sh1.1 bilioni kwa wakazi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ili kusaidia kupambana na umaskini katika kaya zao.

Akizungumza na Mwananchi leo Mei 17,2022 Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi amesema fedha hizo zimetolewa kuanzia Februari 17,2020 hadi Mei 17,2022 kwa wanufaika 7,208 jijini humo.

Makilagi amesema wanufaika wa fedha hizo wamepatiwa mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo ili kubuni miradi ya uzalishaji kwa ajili ya kuongeza kipato cha familia zao.

Amesema baadhi ya wanufaika wa mpango wa Tasaf jijini humo baada ya kupewa mafunzo hayo wameanzisha vikundi vya kukopeshana, biashara ya chakula, kilimo na ufugaji.

"Tunachokifanya sasahivi ni kufanya ufuatiliaji kwa ajili wenye lengo la kujua iwapo fedha wanazopata kutokana na miradi hiyo wanazitumia kwenye masuala ambavyo ni endelevu," amesema Makilagi

Ameongeza; "Fedha hizi zimesaidia kuongeza idadi ya watu wenye shughuli au biashara zenye kuwapatia kipato cha siku na kuwasaidia kumudu gharama za maisha," amesema Makilagi

Advertisement Ofisa Ufuatiliaji wa Tasaf jijini Mwanza, Samson Kagwe amesema mpango huo utaendelea kutoa fedha hizo kwa kaya maskini jijini humo hadi mwaka 2024.

"Matarajio yetu ni kuona jamii inajikwamua kiuchumi kupitia fedha hizi, hatutarajii kuona wanufaika wakitumia fedha hizi katika mambo yasiyo na tija ikiwemo ulevi bila kubuni shughuli mbadala ya kuwaongezea kipato. Kama masharti yatazingatiwa tunaamini utakuwa endelevu zaidi ya mwaka 2025," amesema Kagwe

Mkazi wa mtaa wa Mbugani 'A' jijini hapa, Chausiku Mwaka amesema anapokea Sh48, 000 kila baada ya miezi miwili kutoka kwenye mpango huo.

Amesema fedha hiyo imemsaidia kuanzisha biashara ya kuuza samaki wa kukaanga huku faida ikimsaidia kuhudumia familia yake yenye watoto watatu.

"Mimi ni mjane tangu mwaka 2025. Lakini kupitia biashara niliyoanzisha baada ya kupewa fedha za Tasaf nimefanikiwa kusomesha watoto wangu, wa mwisho yuko Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhale mjini Musoma mkoani Mara, pia mtaji wangu wa samaki umefika Sh250, 000," amesema Mwaka

Naye mkazi wa Kishiri jijini hapa, Zena Philipo amesema fedha hizo zimemsaidia kuanzisha mradi wa kufuga kuku na bata wa nyama ambao anawauza na kupata kipato cha kuhudumia familia yake yenye watoto sita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live