Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanahisa wa TCC wakumbusha gawio

8843 Pic+hisa TZW

Tue, 12 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

 Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) imewatangazia wanahisa wake siku 30 za ukomo wa malipo ya gawio la awali kwa mwaka 2017.

Tangazo hilo linahusu gawio la Oktoba 2017.

Taarifa hiyo inawataka wanahisa ambao hawajalipwa gawio hilo kuwasiliana na matawi ya Posta ili waweze kulipwa kabla ya muda kuisha.

Msimamizi wa mifumo wa kampuni ya CAD Securities inayosimamia malipo hayo, Neemaeli Kitororo alisema endapo mteja atashindwa kufika ndani ya muda uliopangwa atalipwa gawio lake kama madai.

“Atakapoomba kama madai hatopewa kwa uharaka kama ilivyo sasa, itambidi asubiri hadi kampuni itakapofunga hesabu zake au wakati wa kulipwa kwa makundi kulingana na uamuzi wa kampuni,” alisema Kitororo.

Alisema miongoni mwa mambo yanayochangia wanahisa kutofika kwa wakati kuchukua gawio pindi linapotolewa ni kubadilisha mawasiliano tofauti na waliyotumia awali walipokuwa wananunua hisa.

“Wengine walitumia anuani za ofisi wakati wanajisajili na wameacha kazi katika maeneo hayo, wengine walinunuliwa na watu hawajui hata maana yake na wengine wapo vijijini kabisa hakuna mawasiliano mazuri jambo ambalo linawafanya kutokujua kinachoendelea.

(Aurea Simtowe)

Chanzo: mwananchi.co.tz