Benki ya NMB imeidhinisha malipo ya gawio kwa wanahisa ya jumla ya Sh bilioni 143.1.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna alisema mafanikio yaliyopatikana kiutendaji mwaka jana yameipa heshima benki hiyo barani Afrika.
Akiwatangaza kupitishwa kwa gawio hilo jijini Dar es Salaam baada ya kumalizika Mkutano Mkuu wa kila mwaka, Zaipuna aliwaeleza waandishi wa habari kuwa mwaka jana ulikuwa wa mafanikio na kwamba gawio jumla lilikuwa ni ongezeko la asilimia 48 la mkupuo uliotangulia wa Sh bilioni 96.7.
“2022 ulikuwa mwaka wa kihistoria na mafanikio mengi kwa benki yetu. Tukiendelea kujiimarisha katika safari yetu tuliyoianza miaka 25 iliyopita, Benki ya NMB ilipata matokeo mazuri kuwahi kupatikana katika historia yake,” alisema Ruth.