Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanachama wa Ura wakopeshwa Sh458 bilioni

Pic Fedha Data Wastaafu Wanachama wa Ura wakopeshwa Sh458 bilioni

Wed, 28 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya Sh458 bilioni zimekopeshwa kwa wanachama wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Jeshi la Polisi (Ura saccos) tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006.

Kiasi hicho kimetokana na jumla ya mikopo 114,015 iliyotolewa kwa wanachama wake ambao wamenufaika na chama hicho.

Akizungumza Juni 27, 2023 kwenye maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yanayofanyika mkoani Tabora, Meneja Mkuu Msaidizi wa Ura ambaye pia ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Peter Msuya amesema mikopo hiyo imewawezesha wanachama wake kujenga nyumba, kusomesha, kununua vyombo vya usafiri na kufanya maendeleo mengine.

“Mikopo iliyotolewa kwa wanachama mbali ya kuwawezesha kufanya mambo mbalimbali pia imekuza uchumi na kuongeza mzunguko wa fedha nnchini”amesema

Amesema saccos hiyo yenye wanachama 45,000 ina rasilimali za Sh117 bilioni, imepata tuzo za ubora za uendeshaji wa chama akidai misingi ya ushirika inaweza kuwakomboa watu.

Amesema mwaka jana saccos hiyo imetoa mikopo 17,458 yenye thamani ya Sh108.7 bilioni kiwango ambacho ni kikubwa kutolewa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006.

Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk Batilda Burian, Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Dk Rashid Chuachua amepongeza maadhimisho hayo kufanyika mkoa wa Tabora kwa mara ya tatu mfululizo akidai yanaongeza mzunguko wa fedha.

“Mkoa umenufaika kufanyika maadhimisho kwa mara nyingine na wananchi kunufaika kiuchumi,"amesema

Katika maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufungwa Julai Mosi, 2023 yanahudhuriwa na wadau mbalimbali wa ushirika na kuwa na mabanda 150.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live