Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wamlilia JPM malipo yao Nice Catering

JPMS Wamlilia JPM malipo yao Nice Catering

Tue, 28 Apr 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WALIOKUWA wafanyakazi ya Kampuni ya Nice Catering wamemuomba Rais John Magufuli kuwasaidia ili wapelekewe fedha zao katika mifuko ya hifadhi ya jamii, walizokuwa wanakatwa wakati wakifanya kazi katika kampuni hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, kwa niaba ya wafanyakazi wenzake 57, Jumanne Maguzo, alisema wameamua kupeleka kilio chao kwa Rais Magufuli kutokana kuzungumshwa muda mrefu.

Alisema waliachishwa kazi mwaka jana na walipofuatilia fedha za makato ambazo zilipaswa kulipwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii hawajakuta kiasi chochote kilichowekwa na mwajiri wao, wakati walikuwa wanachangia na wanakatwa.

Alisema walikuwa wanakatwa asilimia 10 kwenye mishahara yao kwa mujibu wa sheria.

“Mimi nimefanya kazi miaka tisa, nimeachishwa kazi naenda kufuatilia malipo yangu ya makato ya wafanyakazi hadi leo hatujapata na tukiuliza ofisini hatupewi ushirikiano,” alisema Magunzo.

Maguzo alisema wamefanya jitihada za kukutana na uongozi wa kampuni ili kupata suluhu, lakini wamegonga mwamba kwani kila wakienda ofisini wanaambiwa viongozi hawapo.

Alisema wanapotumia njia ya kupiga simu ili kupanga siku ya kukutana au kuzungumza na uongozi, wamekuwa wakinyimwa ushirikiano.

Mratibu wa wafanyakazi hao, Sospeter Mtelani, aliiomba serikali kuchukua hatua za haraka katika kutatua tatizo hilo kwani maisha yao yamekuwa magumu.

“Mimi nimeacha kazi nikiwa na cheo kikubwa cha ukurugenzi na mmiliki wa kampuni, Yona Sonelo, tulikuwa karibu sana kama rafiki, amenifanyia hivi sijui hao wengine ingekuaje. Niombe Serikali ichukulie suala hili kwa uzito kwani limetuathiri sana,” alisema Mtelani.

Nipashe lilimtafuta Ofisa Rasilimali Watu wa Kampuni hiyo, Jackson Charles, ili kuelekezea suala hilo, ambaye alisema: “Mimi siyo msemaji wa kampuni, labda nikupatie msemaji ndiyo atakueleza kuhusu suala hilo.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live