Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wamiliki, wanahisa sekta ya madini, gesi kuwekwa wazi

Sat, 27 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Waziri wa Madini Angellah Kairuki ameiagiza kamati ya raslimali za madini, mafuta na gesi asilia nchini (TEITI) kuhakikisha kunakuwapo orodha  maalum itakayoweka wazi taarifa za wamiliki ama wanahisa katika sekta hizo.

Akizungumza leo wakati akizundua kamati hiyo, Kairuki aLIsema  haitakuwa rahisi kuanzisha orodha ya taarifa hizo lakini kwa kuwa kamati hiyo imeundwa kwa mchanganyiko wa wadau mbalimbali ana amini watafanikiwa.

“Hili  nitalisimamia kwa karibu sana, kwa nguvu zangu zote kwa gharama zote lakini kwa kutumia weledi wa utaalam wangu na wenu,”aLIsema na kuongeza:

“Naamini haitakuwa rahisi kuanzisha rejista hii kama tu independent Operator (mwendeshaji anayejitegemea) ameenda katika taasisi kufanya ukaguzi na amepata ukinzani naamini hata hiyo register (orodha) haitakuwa rahisi.”

Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani pamoja na kuwataka wajumbe wa kamati hiyo kuwa wazalendo kwa Taifa, alisema madhumuni ya kuanzisha kwa chombo hicho ni kuhakikisha madini yanapochimbwa nchini yanaacha manufaa kwa wananchi.

“Madini, gesi na mafuta hayaoti tena ndio maana ya kuanzisha chombo hikii ili yanapotoka yaache manufaa makubwa kwa wananchi, hiyo ndiyo mantiki kubwa ya kuanzishwa kwa chombo hiki,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa TEITI ambaye aliwahi kuwa Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh alisema katika kipindi chake cha uongozi angependa washughulike zaidi na kuweka mifumo ya utendaji wa kamati hiyo.

“Ukienda kwenye sheria inazungumza kwamba TEITI inawajibika kutengeneza mfumo wa mawasiliano. Nilisoma ripoti uliyoizindua Mei huyo independent administrator analalamika kwamba anapokwenda kwenye industry hapati corporation (ushirikiano),”alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz