Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wamiliki wa mabasi waonywa kupandisha nauli za mabasi msimu wa sikukuu

Wamiliki wa mabasi waonywa kupandisha nauli za mabasi msimu wa sikukuu

Tue, 26 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Mamlaka ya Uthibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) Kanda ya Nyanya za Juu Kusini nchini Tanzania imesema itawachukulia hatua kali wamiliki wa mabasi ya mikoani watakaobainika kupandisha nauli katika kipindi cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka 2019.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Novemba 25, 2019 Meneja wa Kanda wa Latra, Denis Daudi amesema watakaobainika kuongeza gharama za nauli kiholela haitajalisha ni mpiga debe au kondakta wa kampuni yoyote itakayoandikwa kwenye tiketi ya abiria watawajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Amesema wamejipanga kikamilifu kuhakikisha abiria watasafiri kwa nauli elekezi za serikali kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine na si vinginevyo.

"Tunafanya ufuatiliaji na kuchunguza kwa abiria kama wanakata tiketi kwa bei elekezi ya serikali na kama tutabaini kuna nauli inayozidishwa kwa maslahi ya watu wachache hatua stahiki zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na faini ya papo kwa papo," amesema.

Aidha  Daudi amewataka abiria kukata tiketi katika ofisi za mabasi ya kampuni wanazohitaji kusafiria hususan kwa hutumia mitandao ya simu za mkononi ili kuepukana na utapeli unaoweza kujitokeza.

Chanzo: mwananchi.co.tz