Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wamachinga wote Kariakoo kulipa kodi

Fedhapic Wamachinga wote Kariakoo kulipa kodi

Mon, 12 Dec 2022 Chanzo: Mwananchi

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza kuwasajili wafanyabiashara wadogo ‘wamachinga’ waliopo katika Soko Kuu la Biashara Kariakoo.

Akizungumza na wanahabari leo Jumatatu Desemba 12, 2022 Meneja wa Mkoa wa Kikodi, Alex Katundu amesema tayari machinga 5273 wameshasajiliwa ili kuingizwa kwenye mfumo wa malipo ya kodi wa makadirio.

“Usajili huu unafanyika kwa kila machinga aliyepo Kariakoo kwa sababu tulibaini baadhi ya wafanyabiashara wengine sio waaminifu, haonekani akifanya biashara ila mizigo yake anaisambaza kwa machinga ili akwepe kodi. “Lakini tunawasajili baada ya kujiridhisha kwamba wote wanaingiza mapato zaidi ya Sh4milioni kwa mwaka, kuna mapato mengi yanapotea hivyo wataanza kulipa kodi” amesema Katundu.

Usajili huo ulioanza Februari mwaka huu, unafanyika ikiwa ni utekelezaji wa tangazo la Kamishna wa TRA la Julai mosi mwaka huu, linaloagiza kila machinga kusajiliwa eneo hilo.

Chanzo: Mwananchi