Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wamachinga waishukuru serikali

Ef6e47c819be62e937ef2c1bf3492761.jpeg Wamachinga waishukuru serikali

Sun, 2 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wamamchinga katika soko la Buhongwa wameipongeza serikali kwa kukamilisha ujenzi wa kituo cha magari karibu na eneo lao la biashara na kufanya mzunguko wa fedha kuwa mkubwa.

Wito huo umetolewa jana na wafanyabiashara hao katika kipindi hiki cha sherehe za mwaka mpya katika soko la Buhongwa na kusema kuwa wamepata uhakika wa kufikiwa na wanunuzi wa bidhaa zao kutoka maeneo tofauti.

Mfanyabiashara wa matunda na mboga za majani katika soko hilo, Mwajuma Hamis alisema kwa sasa anapata mauzo mazuri kwa siku hali iliyomfanya kuwa na imani kubwa ya kufanya biashara yake hapo.

“Zamani wakati tunakuja hapa hatukutegemea kuwapata wateja kumbe kila kitu mwanzoni huwa na changamoto zake lakini baada ya kutengenezewa miundombinu rafiki na kupatikana kwa kituo cha magari sasa tunashukuru kwa kuweza kupata wateja wengi kila siku,”alisema Hamis.

Mfanyabiashara wa nguo katika eneo hilo, Maziku Malulu alisema kipindi hiki cha sherehe mauzo yameongezeka, hivyo alipongeza serikali kwa kuwatengenezea eneo la kusimama magari karibu na soko lao.

Kujengwa kwa kituo hicho karibu na eneo la wafanyabiashara hao kumefanywa na Kampuni ya Jassie(JASCO) na kuwezesha magari yafikapo katika eneo hilo kuwa na eneo pana la kusimama na kupakia mizigo.

Meneja wa mradi wa Kampuni ya JASCO, Rashid Abdallah alisema wamekamilisha kazi ya ujenzi wa kituo hicho kwa kiwango kilichotakiwa, hivyo alishukuru serikali kwa kuwatumia katika kazi zao.

Aliongeza kusema kuwa watahakikisha wanaendelea kufanya kazi kwa ubora wa namna wanavyoelekezwa na taasisi za serikali.

Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Sekiete Yahaya alisema kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho cha magari ya abiria ni mwendelezo wa uboreshaji wa maeneo ya wafanyabiashara hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live