Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wamachinga kupewa vitambulisho 59,000 kielektroniki

16be7728d0afd70a3d1b9bc3ea97f049.jpeg Wamachinga kupewa vitambulisho 59,000 kielektroniki

Tue, 16 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

UONGOZI wa Mkoa wa Tabora kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanajiandaa kuanza kusambaza kielektroniki vitambulisho 59,000 vya wafanyabiashara wadogo maarufu kwa jina la wamachinga.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Peres Magiri alisema hayo jana wakati akifungua kikao cha kupeana utaratibu wa kusambaza vitambulisho hivyo.

Magiri alisema Halmashauri ya Wilaya ya Igunga imepangiwa vitambulisho 7,670, Halmashauri ya Wilaya ya Nzega vitambulisho 9,440, Nzega Mji vitambulisho 9,440 na Uyui vitambulisho 9,440.

Alisema Manispaa ya Tabora imepangiwa vitambulisho 9,440, Sikonge vitambulisho 4,130, Urambo vitambulisho 4,720, na Kaliua itapata vitambulisho 4,720.

Meneja wa TRA Mkoa wa Tabora, Thomas Masese alisema mfanyabiashara mdogo anatakiwa kuwasilisha maombi kupitia tovuti ya Ofisi ya Rais, Tawala Mikoa na Serikali za Mitaa na kwa watakaoshindwa kujisali kwa njia hiyo wafike ofisi za halmashauri zao.

Masese alisema mwombaji baada ya kukamilisha usajili atapewa namba ya malipo kwa ajili ya ada ya kitambulisho ambayo ni Sh 20,000. Alisema wafanyabiashara hao watapaswa kulipa kwa njia ya benki au simu za mkononi.

Alisema baada ya TRA kupokea maombi itachapisha vitambulisho na kuvipeleka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambaye naye atavipeleka kwa wakuu wa wilaya nao watawakabidhi wakurugenzi watendaji.

Masese aliwataka wafanyabiashara ambao mitaji yao imekuwa na mauzo yanayozidi 10,500 kwa siku wasichukue vitambulisho hivyo badala yake wafuate utaratibu wa kupata leseni za biashara.

Ofisa Biashara Mkoa wa Tabora, Alex Mhanga alisema mwaka 2018/19 walipata vitambulisho 65,000 ambavyo vilitolewa vyote na kuwezesha kupatikana kwa Sh bilioni 1.3.

Mhanga alisema mwaka jana mkoa huo ulipata vitambulisho 71,500 na walivisambaza 60,390 zikapatikana Sh bilioni 1.2. Alisema mwaka jana vilibaki vitambulisho 11,110.

Chanzo: www.habarileo.co.tz