Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wamachinga Mwanza waandamana kumpongeza JPM uamuzi 'Lockdown'

WhatsApp Image 2020 05 19 At 1.webp Wamachinga Mwanza waandamana kumpongeza JPM uamuzi 'Lockdown'

Tue, 19 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyabiashara ndogondogo (Wamachinga) Mkoa wa Mwanza wamefanya maandamano ya kumpongeza Rais John Magufuli kwa mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona tangu uingie nchini na maamuzi yake ya kutowaweka Watanzania kwenye zuio la kutotoka nje (Lockdown).

Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa Wafanyabiashara hiyo Jijini Mwanza, Said Tembo na Joseph Mwita wakizungumza na waandishi wa habari wamesema wanaobeza hatua ya Rais Magufuli ya kuwataka wananchi kuendelea kufanya kazi wapuuzwe.

Tembo, amesema wamachinga wanamuunga mkono Rais Dk. Magufuli kwa uamuzi wake mgumu na msimamo wa kutowaweka Watanzania kwenye zuio kwani alitambua umuhimu wa wananchi wake na kuwathamini .

Amesema kuwa Rais Magufuli ameamini na kumtanguliza Mungu katika mapambano ya corona kuliko binadamu wenyewe na kuna baadhi watu walitabiri Watanzania wengi watakufa kwa ugonjwa huo lakini hadi leo bado wengi wanadunda.

“Wapo wanaombeza Rais Magufuli kuwa hakufanya jambo la busara kutowaweka Watanzania kizuizini hatupingi na tunatambua ugonjwa huo upo na hata yeye juzi akiwa Chato Kanisani alisema katika kupambana na ugonjwa huo kila mtu anatumia mbinu yake....Hivi ukikaa ndani siku nne tu biashara hii ya kuingiza na kutoa mguu ndio ule hali ingekuwaje,”alihoji Mwenyekiti huyo wa Machinga.

Ameeleza kuwa laiti ingetokea Tanzania ingewekwa Karantini hakuna Mfanyabiashara mdogo au mwananchi wa kipato cha kawaida mwenye bajeti ya kumudu kuendesha maisha kwa mwezi mmoja hivyo Watanzania wana kila sababu ya kumpongeza na kumuunga mkono Rais Magufuli, amewawezesha kuendelea kuchapa kazi.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Shirika hilo la Machinga, Joseph Mwita amesema wanamshukuru Rais Magufuli kwa alichokifanya kwa kuwatoa hofu wafanyabiashara na watanzania kuwa hakuna mtu wakufungiwa ndani huku akiwataka waendelee kufanya kazi kwa kujiamini ingawa corona ipo.

“Ametoa takwimu za mambukizi ya ugonjwa huo,ameyakabidhi maisha ya wananchi na taifa kwa Mungu hivyo na sisi tumkabidhi kwa Mungu ampe maisha marefu huku tukichukua tahadhari na kufuata maelekezo ya serikali na wataalamu wa afya,”amesema Marwa.

Aidha, Mjasiriamali katika Soko Kuu la Mwanza, Ester Mgaya amesema hawana budi kumshukuru Mungu lakini pia Rais kwa uamuzi wake mgumu wa kuwatoa hofu watanzania wasitishwe na corona yakuwa hali ikiendelea hivi ataruhusu vyuo vifunguliwe na kushauri kuendelea kumwomba Mungu ili corona itokomee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live