Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliotelekeza vibanda vya biashara Mawasilino warejea

Vibanda Wafanyabiashara (600 X 346) Waliotelekeza vibanda vya biashara Mawasilino warejea

Wed, 11 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyabiashara waliotelekeza vibanda vyao katika Soko la SIMU 2000 mkoani Dar es Salaam, wameanza kurudi kutokana na maboresho yaliyofanyika.

Mfanyabiashara katika soko hilo, Charles Goodluck amesema ili kupata maoni yake kutokana na maboresho yanayoendelea sokoni hapo.

Amesema wafanyabiashara wameanza kurejea kwa kuwa waliondoka sababu soko hilo halikuwa na mazingira rafiki hususan katika kipindi cha mvua.

Katika hilo, ameipongeza Manispaa ya Ubungo kwa Ushirikishwaji wa wafanyabiashara juu ya namna bora ya kuboresha soko hilo kwa kuzingatia mahitaji yao ambapo vibanda vilivyojengwa vinamuwezesha mteja kufika kwenye kila kibanda kutokana na jinsi vilivyojengwa.

Naye Ofisa Mfawidhi kutoka Manispaa ya Ubungo, sehemu ya biashara na masoko, Geofrey Mbwama amesema hatua hiyo ni katika kutekeleza sera na maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha masoko yanaboreshwa.

Amesema kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Manispaa ya Ubungo imeweza kutenga zaidi ya Sh bilioni mbili ambazo ni za mapato yake ya ndani kwa ajili ya uboreshaji wa masoko ikiwemo soko la Mabibo, soko la SIMU 2000, soko la Manzese na soko la Mbezi Shule ili kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live