Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walionguliwa na bidhaa soko la Kariakoo walia na wateja

Kariakoo.jpeg Walionguliwa na bidhaa soko la Kariakoo walia na wateja

Wed, 18 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni zaidi ya mwezi mmoja sasa tangu soko kuu la Kariakoo kuteketea kwa moto, wafanyabiashara wa soko hilo ambao walihamishwa katika masoko ya machinga Complex na Kisutu bado wanakumbana na hali ngumu yakufanya biashara zao.

Kukosekana kwa wateja, kushusha na kupakia bidhaa katika ameneo yao mapya na mazingira wasiyo yazoea yamechangia biashara kuwa mbaya.

Wafanyabiashara wengine wa zamani katika soko hilo ambao walizoea kufanya biashara zao wanasema wamepoteza kazi kwa kushindwa kupata mitaji.

Mfanya biashara mmoja wa pembejeo za kilimo Hussein Kambi alisema kabla ya wao kuoneshwa shehemu maalumu za kufanyia biashara zao, serikali ilitakiwa kuwaandalia sehemu maalumu zakufanyia.

"Mazingira hapa sio rafiki kwetu kuweza kuonyesha bidhaa zetu baada ya masaa ya kufanya biashara hapa kuisha" amesema Hussein.

Mwezi july 27, mwenyekiti wa kamati Liberatus Sabas iliyoundwa kuchunguza chanzo cha moto huo ilikabidhi ripoti hiyo kwa Waziri Mkuu na yaliyobainika na kamati hiyo hadi sasa hayajawekwa wazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live