Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walima mpunga sasa waomba mashine kuvunia

11570 Mpunga+pic TanzaniaWeb

Tue, 17 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Wakulima wa mpunga katika tarafa ya Pawaga na Idodi Wilaya ya Iringa vijijini wanakabiliwa na ukosefu wa mashine za kisasa za kuvuni, jambo linalosababisha zao kupotelea shambani wakati wa uvunaji.

Walizungumza hayo wakati wa ziara ya mwakilishi kutoka Shirika la Chakula Duniani (FAO) nchini, Fredy Kafeero yenye lengo kukagua miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).

Mwenyekiti wa skimu ya umwagiliaji Mkombozi, Salehe Mohammed alisema miundombinu ya kuvunia ni duni, vifaa hakuna hivyo wanalazimika kufyeka na kusababisha mpunga kupotolea shambani.

Naye mwenyekiti wa kikudni cha Tuungane, Twalib Ubwa aliomba shirika hilo kuwajengea uwanja wa kuanikia mpunga iwapo watapata mashine za kuvunia.

Akizungumzia maombi hayo, Kafeero alisema kazi yao ni kuchukua changamoto za wakulima na kuzifanyia kazi.

“Wakulima wana changamoto nyingi na tupo hapa kuzitatua tutahakikisha tunawapayia mashine za kuvunia ili kuokoa upotevu wa mpunga shambani na kuboresha miundombinu ya skimu za umwagiliaji,” alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz