Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima wavuna mabilioni mauzo ya mbaazi

Mbaazi Wakulima wavuna mabilioni mauzo ya mbaazi

Mon, 18 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakulima wa zao la mbaazi ghafi mkoani Lindi wamepata Sh bilioni 32.8 msimu huu.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Terack amesema hayo leo Septemba 18, 2023 wakati akitoa taarifa ya mkoa mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa hadhara sanjari kuweka Jiwe la Msingi katika barabara itokayo Nanganga Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara hadi Ruangwa Lindi.

Amesema miaka ya nyuma wakulima wa zao hilo walikuwa wanauza mbaazi ghafi kwa Sh 2000 kwa kilo moja.

Amefafanua baada ya kukubaliana na Wizara ya Kilimo kwa kuridhia kuuzwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani kilo moja iliangukia Sh 2000 hadi Sh 2005.

RC huyo ameeleza kuwa zao la ufuta wakulima waliweza kupata Sh bilioni 98 msimu huu. Aliongeza zao la korosho limeweza kuuza Sh bilioni 106 msimu uliopita.

Aidha mkoa ilijiwekea mkakati kuweza kuzalisha zaidi mazao hayo. Ameongeza ile tabia kuwa zao la mbaazi ni mboga sasa ni biashara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live