Wakulima wa Wilaya ya Ruangwa, Nachingwea na Liwale, wakiongozwa na wenzao kutoka kijiji cha Kitogoro, wilayani Liwale Mkoani Lindi wamesema bei za Korosho zilizotajwa kwenye minada ni ndogo ila imewabidi wauze kwa kuwa hawana namna nyingine
Wakulima hao wameiomba serikali kubuni mbinu mbadala iwasaidie kuuza korosho zao kwa tija.
Katika kijiji cha Kitogoro ambapo mnada wa 3 unafanyika kwa niaba ya wakulima wengine wote wanaounda umoja wa Runali, Wakulima wanakiri bei kuongezeka katika mnada huu wa tatu ila kwa msimu wanasema hali ni mbaya kwani Korosho zinashuka mno
Wanasema kuwa shughuli wanazozifanya katika kuandaa mashamba na kuokota korosho hizo ni za gharama mno, lakini bei wanayokuja kuuzia korosho zao inakatisha tamaa.
Huu ni mnada wa tatu kwa umoja huu wa Runali yani Ruangwa, Nachingwea na Liwale, lakini ni mnada wa Pili wakulima kukubali kuuza.
Kwa umoja wao wameuza Korosho zaidi ya Tani Elfu Tano. Lakini Minong’ono ya baadhi yao ni kwamba endapo bei haitakaa sawa kwa msimu huu basi dhamira yao ni kuacha kabisa kuuza korosho mnadani na kuona ni kheri wakaange na kuuza mitaani.