Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima watarajia kuvuna tumbaku ya bil 53/-

Dd0177924f11734fcd0ecf03dc0c119f Wakulima watarajia kuvuna tumbaku ya bil 53/-

Wed, 27 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

CHAMA Kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa Tumbaku Kanda ya Magharibi (WETCU) kupitia vya ushirika vya mazao (AMCOS) katika msimu wa kilimo wa mwaka 2020/2021 kinatarajia kuzalisha kilo milioni 14 za tumbaku zinazotarajiwa kuwa na thamani ya Sh bilioni 52.5.

Meneja wa WETCU, Samweli Jokeya alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu kufanyika tathmini ya uzalishaji wa kilo za tumbaku msimu wa kilimo wa 2020/2021.

Jokeya alisema kilo milioni 14 zitakazozalishwa msimu huu zinatokana na AMCOS 91 zilizothibitisha uzalishaji wa zao hilo na kwamba Sh 52,582,600,000 zitapatikana.

Alisema makisio hayo ni kabla ya Januari, 2021 na hali ya vyama AMCOS ya uchukuaji mbolea uliendelea vyema.

Alisema kuna vyama ambavyo awali vilikuwa vinasubiri mbolea yote lakini kuna vingine vilichukua kwa awamu. Alisema tangu msimu huu ulipoanza kulikuwa na asilimia 50 tu ya wakulima wa tumbaku waliokuwa wakichukua mbolea kwa kusuasua wakiwemo waliosubiri mbolea yote kwa mkupuo, lakini kwa sasa hali ya uchukuaji imeimarika.

Jokeya alisema WETCU kupitia wataalamu wa kilimo wameendelea kutoa elimu kwa wakulima wa zao hilo kutumia viuatilifu kudhibiti wadudu wanaoharibu mimea ya tumbaku.

Alisema pia wanatoa elimu wapande na kuhudumia tumbaku kwa kukizingatia upandaji miti.

Chanzo: habarileo.co.tz