Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima watakiwa kupima afya ya udongo

113d56d6b782772103e82e899e7ea3ca Wakulima watakiwa kupima afya ya udongo

Wed, 3 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakulima jijini Dar es Salaam, wameshauriwa kupima afya ya udongo, kabla ya kuanza kilimo kwa sababu inasaidia kujua changamoto zilizopo na kupatiwa ufumbuzi stahiki.

Ushauri huo umetolewa na mtaalam wa kilimo kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Emmanuel Massanja alipokuwa akionesha teknolojia ya upimaji udongo kwa wananchi mbalimbali waliofika kwenye maonyesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki 2022 yanayofanyika mkoani Morogoro.

Massanja alisema katika kilimo ni lazima kujua tabia za udongo, ambazo zipo katika makundi ya kifizikia, kikemikali na kibaiolojia, ili mkulima aweze kunufaika na kilimo kwa ajili ya kujiongezea kipato.

Alisema halmashauri hiyo ina maabara ndogo katika shamba darasa lililopo eneo la Pugu Kinyamwezi, jijini Dar es Salaam, ambayo wataalam wapo kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi.

Alisema kupitia maabara hiyo, wakulima wanaelimishwa jinsi ya kuchukua udongo shambani na kupimwa, ili kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Majaliwa Andrea aliwataka wananchi kutumia fursa zilizopo katika ardhi iliyopo ili kuinua uchumi binafsi na taifa kwa ujumla.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live