Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima wataka zao la kahawa kupewa kipaumbele

Kahawa Pc Wakulima wataka zao la kahawa kupewa kipaumbele

Thu, 14 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakulima wa zao la Kahawa wilayani Kalambo Mkoani Rukwa wameiomba serikali kuwekeza katika kilimo cha zao hilo ili kuwawezesha kuondokana na kilimo cha mazoea na kufanya zao hilo kuwa kubwa na la biashara 

Wameiomba serikali kutoa ruzuku na mbegu za kutosha ili wazalishe zao hilo kwa tija

Wakiongea katika nyakati tofauti tofauti wakulima wilayani humo wamesema Serikali haina budi kuwekeza zaidi katika zao la kahawa kwa kutenga bajeti kila mwaka kwa ajili uendeshaji wa zao hilo ambalo litasaidia kujikwamua kiuchumi kutokana na soko lake kuwa kubwa nal auwazi duniani.

Akiongea na wakulima wilayani humo Kaimu Afisa kilimo wilayani Kalambo Elieza Stephen, amesema katika msimu wa kilimo wa mwaka 2021/2022 zaidi ya hekali 30 zimepandwa na Serikali kutoa ruzuku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live