Dodoma. Wasambazaji wa pembejeo za wakulima nchini wamemweleza Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga hali ngumu wanayokumbana nayo kutokana na Serikali kutowalipa Sh36.9 bilioni.
Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha Wazalishaji, Wasambazaji wa pembejeo za Kilimo na Mifugo, Gerald Mlenge ametoa kauli hiyo leo Septemba 19, 2019 kwenye mkutano wa wadau wa kilimo mjini Dodoma.
"Wenzetu 13 wameshatangulia mbele za haki, tunaomba fedha zetu Sh36.9 bilioni tulipwe kama kuna makosa kwa nini tusipelekwe katika vyombo vya dola, tusaidie kuonana na Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa)tumwambie," amesema Mlenge.
Amesema kumekuwa na ucheleweshwaji wa wa kulipwa madai jambo linalowakatisha tamaa na baadhi wanapoteza maisha kwa sababu ya mawazo.
Hata hivyo, Hasunga ametaja sababu za kuchelewesha malipo hayo kuwa ni udanganyifu kwa kuwa kulikuwa na malipo hewa asilimia 80.
Waziri huyo amesema wakati wowote Serikali itawafikisha mahakamani waliofanya udanganyifu huo ili sheria ichukue mkondo wake.
Pia Soma
- Mwanasiasa jela miaka sita
- IGP Sirro mwenyekiti mpya shirikisho wakuu wa polisi Mashariki mwa Afrika
- Kenya kuzalisha umeme wa nyukilia