Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima washauriwa kuongeza thamani mazao yao

Wakulima Wa Mpunga Wapata Hasara Ya Mamilioni 1536x1028 Wakulima washauriwa kuongeza thamani mazao yao

Sun, 13 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela amewataka wakulima na wafanyabiashara kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuongeza thamani katika mazao yao ili yaweze kujulikana kimataifa na kupata soko.

Mongela ameyasema hayo jana Jumamosi Jijini Arusha wakati akifungua maonesho ya kimataifa ya kilimo yanayojulikana Kama "TANZFOOD Expo amesema maonyesho hayo yanalenga kukuza sekta ya kilimo

Mongella amewataka wakulima kuyatumia maonyesho hayo kujifunza masuala mbalimbali ili waongeze ujuzi wa namna bora ya kuongeza thamani mazao yao ili waweze kukuza fursa ya soko.

"Nimeweza kutembelea maonesho haya na kujionea mazao mbalimbali huku nikipata elimu ya kutosha kutoka kwa nchi za wengine namna ambavyo wameweza kuboresha katika utalaamu wa kilimo, ufugaji pamoja na uchakataji na hii ni fursa kwao kujifunza zaidi ."amesema .

Mmoja wa Wakurugenzi wa KILIFAIR Promotion, Dominic Shoo amewaomba wananchi mbalimbali kutembelea maonesho hayo kwa ajili ya kujifunza pamoja na kufanya biashara pia kukutana na wadau wa kilimo katika kubadilishana mawazo ikiwemo kubadilishana changamoto na fursa.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Christophe Bazivamo amepongeza uwepo wa maonesho hayo ambayo yatakuza mnyororo wa thamani katika sekta ya kilimo kutokana na uzalisha uliopo kwenye viwanda katika jumuiya ya Afrika ya mashariki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live