TUME ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) imesema tani trillioni 1.009 za mazao ya kimkakati ya tumbaku, kakao, pamba , chai , ooya , choroko , korosho , kahawa, mkonge na dengu yaliunzwa kupitia vyama Vya ushirika ,ambapo jumla ya Sh trillioni 2.9 zililipwa kwa wakulima kati ya mwaka 2021/2022 hadi 2022/2023.
Mrajisi wa Vyama vya Ushirika , Dk Benson Ndiege amesema hayo Mei 17, 2023 mjini Morogoro kwenye taarifa yake kabla ya Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro, Dk Mussa Ali Mussa kufungua mafunzo ya usimamizi wa vyama vya ushirika katika Kanda ya Mashariki kwa maofisa 78 wa ushirika wa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.
Dk Ndiege ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa TCDC amesema , Tume hiyo hadi sasa inasimamia Vyama vya Ushirika 7,300 vyenye wanachama takribani milioni 12 katika sekta mbalimbali ikiwemo , kilimo, mifugo , uvuvi , madini, nyumba , fedha , biashara ndogo na nyinginezo.
Mrajis wa vyama vya ushirika nchini amesema licha ya mauzo ya tani hizo na kiwango hicho cha fedha kilicholipwa kwa wakulima , kwa mwaka 2021/2022 serikali kupitia Mamkala za Serikali za Mitaa ilipokea jumla ya Sh bilioni 15. 144 zikiwa ni fedha za ushuru utokanao na zao la korosho pekee, kwa mikoa ya Lindi na Mtwara.