Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima waitaka Serikali kuacha kuagiza mahindi nje

52953 WAKULIMA+PIC

Thu, 18 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nairobi, Kenya.Wakulima nchini Kenya wameionya Serikali dhidi ya uagizaji wa mahindi ili kutosheleza mahitaji ya bidhaa hiyo nchini humo.

Wakulima hao wamesema hawatakubali wizara ya kilimo kuagiza mahindi kwa kuwa hatua hiyo itawaharibia soko.

Wakulima hao pia wameitaka Serikali kusaidia wakulima badala ya kuwatajirisha wachache.

Aidha, wakulima hao wametaka kuwa na uwakilishi  kwenye kila jukwaa linalozungumzia masuala ya kilimo.

Wamesema wasagaji wa unga wamekuwa wakitoa bei nzuri kwa mahindi yao pamoja na wafanya biashara wa kibinafsi kuliko Serikali.

Juzi  gunia moja la kilo 90 lilikuwa likiuzwa kwa Sh 3,200.



Chanzo: mwananchi.co.tz