Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima, wafugaji wapewa tahadhari mvua za El-Nino

Maji Ya Mvua.jpeg Wakulima, wafugaji wapewa tahadhari mvua za El-Nino

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na wataalamu wa sekta husika wametoa tahadhari na ushauri kuhusu mwenendo wa mvua za vuli na zile za El Nino zinazotarajiwa kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini kuanzia Novemba 2023 hadi Aprili 2024.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Ladislaus Chang’a amesema katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi na usalama wa chakula, vipindi vya unyevu wa kuzidi kiasi pamoja na mafuriko vinaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji wa mazao na miundombinu ya kilimo.

Amesema magonjwa kama vile ukungu yanatajarajiwa kuongezeka na kuathiri mazao kama viazi mviringo, nyanya, ufuta na maharage.

Kufuatia hali hiyo Dkt. Chang’a amewashauri Wakulima kuendelea na shughuli za kilimo kama kawaida hususan katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi Juu ya wastani.

Kwa upande wa mifugo na uvuvi amesema milipuko ya magonjwa ya mifugo kama vile ugonjwa wa homa ya bonde la ufa, midomo na kwato, na kuzaliana kwa wadudu wanaosambaza magojwa yanaweza kujitokeza.

Vilevile kunaweza tokea matukio ya kuongezeka kwa magonjwa ya mwani baharini na kupungua kwa uzalishaji wa mwani kutokana na kupungua kwa kiwango cha chumvi ya maji ya bahari.

Kwa Wakulima wa mwani, TMA imewashauri kulima mwani kwenye maji ya kina kirefu ili kuondokana na athari za maji ya mvua yanayokuwa yanaingia baharini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live