Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima, wafugaji wahimizwa bima ya mazao, mifugo

NYUKI KILIMO Wakulima, wafugaji wahimizwa bima ya mazao, mifugo

Wed, 3 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakulima nchini wameshauriwa kuchangamkia bima ya mazao na mifugo ili kuwasaidia kuongeza uzalishaji na kulima au kufuga bila hofu.

Ofisa Uhusiano wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Euphrasia Mawalla alisema hayo katika mahojiano maalumu na HabariLEO kwenye maonesho ya Nanenane yanayoendelea kitaifa mjini Mbeya.

Alisema wakulima na wafugaji ambao wamechangamkia bima wamenufaika pale walipokutwa na majanga na hivyo mkulima akitaka kulima na kulala raha mustarehe akate bima ya mazao yake.

Alitoa mfano wa wakulima wa korosho ambao waliwekea bima mazao yao na kupata hasara ya korosho kunyauka ambao kwa mwaka 2021/2022 wamelipwa shilingi milioni 220, ili kufidia hasara zao.

Alitaja wakulima wengine walionufaika na bima kuwa ni wale wa mpunga wa mkoani Morogoro ambao hivi karibuni wamelipwa Sh milioni 21 kufidia hasara mbalimbali walizopata.

Mratibu wa Bima za Mazao na Mifugo wa NIC, Prosper Peter, alitaja faida za kukata bima ya mazao au mifugo, mbali na kukuza biashara kuwa ni pamoja na kuweza kukopesheka kwenye benki mbalimbali.

Alifafanua kwamba benki zimekuwa zikisita kuwakopesha mitaji wakulima na wafugaji zikihofia fedha zao kushindwa kurudi kutokana na hasara inayoweza kuwapata wakulima au wafugaji kutokana na ukame, mafuriko au magonjwa.

“Lakini mtu akishakuwa na bima, benki inakuwa na hakika kwamba endapo ikitokea hasara itarejesha fedha zake,” alisema.

Alitaja faida kubwa ya bima ni kumrejesha mkulima au mfugaji kwenye hali aliyokuwa kabla ya mifugo au mazao yake kukumbwa na majanga.

Alisema malipo ya mwaka ya bima ya mifugo ni asilimia tano ya thamani ya ng’ombe wa maziwa na asilimia nne kwa thamani ya ng’ombe wa nyama.

Kwa mifugo alisema bima hulipwa kwa kuangalia asilimia nne mpaka sita ya thamani ya uwekezaji kwenye shamba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live