Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima wafichua kutoa taarifa za uongo zilivyowakosesha pembejeo

Mwenyeji Korosho Wakulima wafichua kutoa taarifa za uongo zilivyowakosesha pembejeo

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakulima wa korosho mkoani Mtwara wamekiri kutoa taarifa za uongo wakati wa uandikishaji wa wakulima ili wapatiwe pembejeo wakihofia kudaiwa ushuru.

Zoezi la uandikishaji wa wakulima lilizinduliwa Januari mwaka huu ambapo likiwa na lengo la kusajili zaidi ya wakulima wa zao la korosho 400,000.

Akizungumza na Mwananchi kijijini hapo, Munda Hassan Mkulima Naguruwe amesema kuwa katika zoezi uandikishaji pembejeo wakulima wengi wengi walidanganya serikali na kutoa taarifa ambazo siyo sahihi.

“Kwa mfano mimi na miliki hekali 10 lakini kwenye uandikishaji nilisema nna hekali 2 baada ya kuja pembejeo nimepata mfuko mmoja jambo hili limenigharimu sana tulidhani tutalipishwa ushuru hivyo wengi tulipata hofu,” amesema.

“Huenda tungesema ukweli tungepata pembejeo stahiki kwa hili limetugharimu tunaomba Serikali iturekebishie ili msimu ujao tupate pembejeo za kutosha stahiki,” amesema Hassan.

Rehema Said Hamis Mkazi wa Nanguruwe alisema kuwa kwa sasa tatizo ni kubwa kuhusu dawa wengine tulijiandikisha na vitambulisho tunavyo lakini havisomi kwenye mfumo.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Nanguruwe, Coloa Salum Coloa amesema kuwa elimu kubwa inatakiwa ili kuwasaidia wakulima kwakuwa wengi wao walirubuniwa na kupewa taarifa ambazo siyo stahiki.

“Tatizo Serikali haikutoa elimu yaani haikuipita kwa wakulima vyakutosha ambapo wengi waliambiwa kuwa kuna watu watapita kuandikisha mashamba bila kuweka wazi nini kinaenda kufanyika baada ya uandikishaji,” amesema.

Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania, Francis Alfred amesema kuwa wakulima ambao walitoa taarifa ambazo siyo za kweli watatakiwa kuboresha taarifa zao wakati wa zoezi la uhuishaji wa kanzi data ili waweze kupata pembejeo katika msimu ujao.

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Masasi & Mtwara, Siraji Mtenguka amesema kuwa kabla ya zoezi la uandikishaji chama kilipita kutoa elimu na kuwaeleza umuhimu wa zoezi hilo.

“Licha ya elimu hiyo lakini wapo ambao hawakutaka kabisa kujiandikisha lakini wapo ambao walifupisha taarifa zao hali ambayo imesababisha kupata pembejeo kidoogo tofauti na ukweli wenyewe,” amesema Mtenguka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live