Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima wa zabibu Dodoma wapewa somo

25287 Zabib+pic TanzaniaWeb

Sun, 4 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

 Dodoma. Naibu Waziri wa Kilimo,  Omary Mgumba amewakata wakulima wadogo wa zabibu mkoani Dodoma kujiunga katika vyama vya ushirika ili kuepuka kupata hasara kwa mazao yao kuozea shambani.

Mgumba ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Novemba 3,2018 wakati akizungumza katika uzinduzi wa tamasha la mvinyo ambalo ni la kwanza kufanyika nchini.

Amesema wakulima wanapata hasara kwa kuwa wanunuzi hawajui wapi pa kupata zabibu, lini wanaipata na kwa bei ipi.

“Wakulima wakubwa hawana tatizo hili kwa kuwa wanunuzi wanawajua ila tatizo lipo kwa wakulima wadogo kufikiwa na wanunuzi. Wakijiunga kwenye vyama itarahisisha kwa kuwa zabibu itakuwa inakusanywa sehemu moja na kuuzwa kwa  elekezi ya soko," amesema Mgumba.

Hata hivyo, amesema zabibu imeingizwa kwenye mazao ya kimkakati ili kuwafanya wakulima wa zao hilo kunufaika na kujiongezea kipato.

Amesema kuwa kituo cha utafiti cha Makotopora jijini hapa kimepewa jukumu la kufanya utafiti wa zao zabibu.

Waziri mkuu mstaafu, John Malecela amewataka vijana wa Dodoma kuacha tabia la kulia umasikini badala yake waitatue changamoto hiyo kwa kujikita kwenye kilimo cha zabibu.

Amesema kuwa vijana hao wanaweza kukabiliana na umaskini kupitia taasisi zinazowasimamia ili angalau kila kijana awe na nusu eka kwa ajili ya kulima zabibu.

Chanzo: mwananchi.co.tz