Uvinza. Wakulima wa zao la tumbaku wilayani Kigoma wameiomba Serikali kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kupunguza kiwango cha fedha cha kulipia katika mfuko huo.
Ombi hilo limetolewa leo Jumapili Mei 12 na wanachama wa chama cha ushirika cha tumbaku (AMCS) katika kijiji cha Basanza, wakisema wanaomba kupunguzwa kiwango kutoka Sh76, 800 hadi Sh38,400 ili kila mmoja aweze kupata huduma hiyo.
Beatrice Musule amesema wakulima hawawezi kumudu gharama hizo kutokana na wakati mwingine kukosa mavuno kwa sababu ya wadudu wanaoharibu mazao yao.
"Afya ni jambo muhimu na wametuletea wakati mzuri lakini tunaomba Serikali yetu sikivu ituangalie sisi wakulima wadogo wa tumbaku iweze kupunguza kiwango ili tuingie na familia zetu," amesema Masule.
Stephano Guha amesema ni vema wakaliangalia jambo hili kwa mara ya pili na kuwaruhusu kulipia taratibu kwa awamu nne kutokana na umuhimu wa jambo la afya.
"Tutalipa kiasi hicho lakini tunaomba watuwekee utaratibu wa kulipa kwa awamu au watupunguzie kiwango kila mmoja anatamani kujiunga lakini tunashindwa," amesema Guha.
Pia Soma
- Ujumbe wa Dk Bilal katika mashindano ya kuhifadhi Quran
- Ukuta Mirerani wasaidia Serikali kukusanya Sh1.43bilioni
- Walichokisema Chadema wakurugenzi kupigwa ‘stop’ kusimamia uchaguzi
"Nichukue fursa hii kuwahamasisha wakulima kujiunga na mfuko huo kwani ugonjwa ukija hautoi taarifa ni muhimu kila mmoja wetu akawa na kadi ya bima ya afya yeye na familia yake," alisema Hoza.
Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi kuuza mazao yao baada ya kuvuna na kuhakikisha wanaweka akiba ya chakula kwani Serikali haitampatia mtu chakula kwa kufanya uzembe kama huo.
Meneja wa NHIF mkoa wa Kigoma, Benard Katerengabo, alisema wataendelea kutoa elimu kwa wakulima na vyama vya ushirika mkoani humo lengo kila mkulima aweze kunufaika yeye pamoja na familia yake.