Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima wa parachichi Tanzania wala shavu Saudi Arabia

Parachichi.jpeg Wakulima wa parachichi Tanzania wala shavu Saudi Arabia

Thu, 18 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali J. Mwadini amewataka wakulima wa zao la parachichi hasa wale wanaosafirisha kutoogopa usafirishaji wa zao hilo au ushindani wa masoko kwa sababu uhitaji wa Parachichi bado ni mkubwa sana katika nchi ya Saudi Arabia.

Aliyasema hayo akiwa mkoani Njombe huku akiambatana na mwekezaji wa Saudi Arabia ambapo walitembelea kiwanda cha kuchakata na kupakia parachichi zinazosafirishwa nje ya nchi cha “AvoAfrica” kilichopo katika Halimashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe.

Balozi Mwadini alisema “Hatuna haja ya kuogopa ushindani, kwasababu sisi bidhaa zetu hata tukizalishaje hatuwezi kujaza masoko.

Soko la Saudi Arabia hii bidhaa yote ikienda pale inaweza kumalizika, kwahiyo tujitahidi kuzalisha kwa bidii huku tukizingatia ubora ili bidhaa inapokwenda masoko ya nje ijenge taswira nzuri kwa watu kuhusu Tanzania.

Meneja wa kiwanda cha “AvoAfrica”amesema uwezo wa kiwanda hicho ni kusafirisha tani 3800 za Parachichi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live