Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima wa mwani walia bei ndogo sokoni

Mwani Mwaniii Wakulima wa mwani walia bei ndogo sokoni

Thu, 25 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakulima wa Mwani mkoani Tanga waiomba serikali kuingilia kati bei ya zao hilo kwenye soko kwani imeshuka kutoka Sh 1800 hadi Sh 600 kwa kilo.

Malalamiko hayo wameyatoa wakati wa ugawaji wa vitendeakazi kazi vilivyotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi vyenye thamani ya Sh milioni 6.2 kwa vikundi vya wakulima wa zao hilo katika wilaya za Tanga Muheza Pangani na Mkinga.

Wamesema kuwa licha ya kilimo hicho kufanyika kwa gharama kubwa lakini changamoto iliyokuwepo kwa sasa ni malipo kidogo ya mauzo ya zao hilo katika masoko.

"Tunaomba serikali itusaidia kwani bei ya kilo ya mwani mnene ilikuwa Sh 1,800 sasa imefika Sh 1.300 huku mwani mwembamba ili kuwa Sh 1,300 sasa imefika Sh 600 halafu na madalali wanaonunua wanatukopa hivyo mkulima hapati faida"amesema Fatma Rashid mmoja wa wakulima hao.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dk Batilda Buriani amesema atakutaka na makampuni ambayo yamepewa leseni ya kununua mwani wa Mkoa wa Tanga ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo ya wakulima. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live