Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima wa mahindi walivyovuna zaidi ya Sh10,000 kwa gunia Tanzania

Pop Corn 785074 1920 Bei ya mahindi inatajwa kuwapa ahueni ya maisha wakulima

Thu, 7 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakulima wa mahindi nchini Tanzania wamevuna Sh10,876 kwa kila gunia la kilo 100 ndani ya mwaka mmoja uliopita, huku bei ya zao hilo la chakula ikishuka kidogo kwa mwezi mmoja uliopita.

Ripoti ya Mapitio ya Uchumi kwa mwezi Machi 2022 (Monthly Economic Review) iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inaeleza kuwa wastani wa bei ya jumla ya gunia la kilo 100 la mahindi mwaka kwa ulioishia Februari 2022 ilikuwa ShSh62,326 ikiwa imepanda kutoka Sh51,450 iliyorekodiwa kipindi kama hicho mwaka 2021.

Bei hiyo ya Februari mwaka huu ipo juu kwa asilimia 17.5 ikilinganishwa na ya mwaka jana.

Hiyo ni sawa na kusema wakulima wa mahindi wamevuna Sh10,876 kwa kila gunia la kilo 100 mwezi Februari mwaka huu ikilinganishwa na walichouza Februari 2021.

Uchambuzi zaidi wa takwimu hizo za BoT unaonyesha kuwa bei ya zao hilo umeshuka kidogo ndani ya mwezi mmoja uliopita kutoka Sh65,864 Januari hadi hadi ShSh62,326 Februari mwaka huu kwa bei ya jumla.

Kupanda kwa bei ya mahindi kumetokana na kuongezeka kwa mahitaji ya zao hilo sokoni wakati huu ambao wakulima wanaendelea na shughuli za kilimo.

Kupanda kwa bei hiyo kunawaumiza walaji kwa kuwa wanalazimika kutoboa zaidi mifuko yao kupata chakula hicho muhimu na utengenezaji wa bidhaa viwandani.

Kwa wakulima ambao wamewekeza kulima zao hilo, kwao ni kicheko kwa sababu inawaongezea faida ikilinganishwa na bei waliyotumia kuuza mwaka jana.

Bei za mazao mengine ya chakula

Pia katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita unaoishia Februari 2022, bei za mazao yote ya chakula zilipanda isipokuwa maharage.

Bei ya jumla ya maharage kwa Februari 2022 ilikuwa Sh184,175 ikishuka kutoka Sh195,554 iliyorekodiwa kipindi kama hicho mwaka jana.

Hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan alisema bei za bidhaa zote ikiwemo chakula zitapanda kwa sababu ya vita inayoendelea kwa sasa kati ya Urusi na Ukraine ambayo imetatiza mifumo ya kibiashara duniani hasa usafirishaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live