Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima wa korosho wasalimu amri

Korosho Tandahimbaaa Wakulima wa korosho wasalimu amri

Sat, 5 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakulima wa korosho katika Wilayani za Tandahimba na Newala kupitia Chama Kikuu cha Ushirika cha (TANECU) wamekubali kuuza korosho zao kwa bei ya juu ya Sh1, 910 na bei ya chini Sh1, 900 katika mnada wa tatu.

Hatua hiyo imekuja wakati Oktoba 21, 2022 wakulima hao walikataa kuuza korosho zao katika mnada wa kwanza bei ya juu Sh2, 011 na bei ya chini Sh1, 630 na mnada wa pili uliofanyika Oktoba 28 kwa bei za Sh2, 200 na Sh1, 800.

Akizungumza mara baada ya wakulima hao kuuza korosho hizo katika mnada wa tatu uliofanyikia Tandahimba, Mwenyekiti wa TANECU Karimu Chipola amesema kuwa walifikisha sokoni zaidi ya tani 3,575 na zote zimeuzwa.

“Wakulima wengi wa hili zao tunakwenda kwa kuhisi kuwa msimu huu bei ikiwa ndogo basi msimu ujao nitauza sana, kitu ambacho sio sawa hasa kwa mabadiliko yanapojitokeza katika soko la duni,” amesema Chipola.

Katika Mnada wa tatu wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Mazao wa Masasi - Mtwara (MAMCU), wameuza tani 616 kwa bei ya juu 1,945 na bei ya chini 1, 840.

Mwenyekiti wa chama hicho Siraji Mtenguka amesema kuwa Mnada huo umefanyika kijiji cha Narunga, Kata ya Njengwa Halmashauri ya Mji Nanyamba, ambapo amewashukuru wakulima waliojitokeza katika mnada huo kwa kuridhia kuuza korosho zao.

“Unajua hata sisi hatufurahishwi na bei zilizopo sokoni lakkni nikipindi cha mpito tu kikubwa wakulima wanapaswa kuwa wavumilivu na bei iliyopo sokoni,” amesema Mtenguka

Chanzo: www.tanzaniaweb.live