Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Wakulima wa korosho waboreshewe mazingira'

Wakulima Wa Korosho Waboreshewe Mazingira 'Wakulima wa korosho waboreshewe mazingira'

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu Yahya Mhata, ameishauri serikali kuboresha mazingira wezeshi kwa wakulima wa korosho ili waweze kuzalisha kwa wingi. - Akichangia bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu bungeni mjini Dodoma, Mhata amesema changamoto kubwa iliyokuwepo hakuna takwimu sahihi za wakulima wa korosho katika jimbo la Nanyumbu. - Mhata ameishauri serikali kupitia Bodi ya Korosho nchini kuanza kufanya uhakiki wa wakulima wa korosho, ili wote waweze kufaidika na fursa za vitendea kazi zinazotolewa na serikali.

Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu Yahya Mhata, ameishauri serikali kuboresha mazingira wezeshi kwa wakulima wa korosho ili waweze kuzalisha kwa wingi. - Akichangia bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu bungeni mjini Dodoma, Mhata amesema changamoto kubwa iliyokuwepo hakuna takwimu sahihi za wakulima wa korosho katika jimbo la Nanyumbu. - Mhata ameishauri serikali kupitia Bodi ya Korosho nchini kuanza kufanya uhakiki wa wakulima wa korosho, ili wote waweze kufaidika na fursa za vitendea kazi zinazotolewa na serikali. “Bodi ya Korosho wameshindwa hata kuwapatia viatu zile gamboot wale vijana wanakwenda kusajili mashamba ya wakulima wanatumia viatu vyao kipindi hiki cha mvua, vijana hawa wanakwenda kufanya kazi bila miamvuli sasa unaanza kujiuliza lengo la bodi ya korosho ni kupata takwimu sahihi za wakulima au kufunika kombe mwanaharamu apite, “ amesema Mbunge Mhata.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live