Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima wa korosho Kilindi wapewa somo

Dabb18b9d6da4399296e64d78163c66e Wakulima wa korosho Kilindi wapewa somo

Thu, 19 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAKULIMA wa zao la korosho katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga wameshauriwa kufuata kanuni bora za kilimo cha zao hilo ili kuongeza uzalishaji wenye tija na kujipatia kipato.

Ushauri huo ulitolewa hivi karibuni wakati wa mafunzo ya siku mbili ya kilimo bora cha zao hilo ambayo yalitolewa na na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (Tari) Naliendele kwa kushirikiana na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT).

Akizungumzia mafunzo hayo, Ofisa Uhalishaji, Teknolojia na Mahusiano wa Tari Naliendele, Stella Andrea alisema lengo lake ni kuwapatia wakulima wa zao hilo teknolojia mpya za kilimo bora, kutumia mbegu bora na kudhibiti wadudu waharibifu na magonjwa ili ifikapo mwaka 2025 Tanzania iweze kufikisha uzalishaji wa tani milioni moja kwa mwaka kutoka tani 313,000 za sasa.

Akiwasilisha mada kwa washiriki wa mafunzo hayo, Dadili Mjule aliwataka wakilima wa korosho kuendesha kilimo cha kisasa kama vile kuchagua eneo la kupanda mikorosho, kutayarisha shamba vizuri kwa kutifua ardhi, kudhibiti mangojwa na mashambulizi ya wadudu na kuzuia shamba kutokuwa malisho ya wanyama.

Ofisa Kilimo kutoka CBT tawi la Tanga, Frank Futakamba alisema kwa kawaida korosho zikishakomaa huanguka zenyewe nikiwa na mabibo, hivyo ni vyema kuzivuna na kuzitenganisha na mabibo kabla ya kuanguka.

Alisema ni muhimu mkulima kupalilia na kusafisha eneo linalozunguka mikorosho ili kurahisisha uvunaji.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kilindi, Gracian Makota alisema awali wilaya hiyo ilikuwa hailimi zao hilo lakini wakabaini linastawi kwenye ardhi hiyo na msimu wa korosho 2018/2019 walinunua mbegu za kutosha kupandwa kwenye ekari 11,000 ambazo walizinunua kwa ushirikiano wa Tari Naliendele na Kibaha.

Alisema mbegu hizo walizigawa bure kwa wakulima ili kuwahamasisha kuanza kulima zao hilo.

Chanzo: habarileo.co.tz