Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima wa embe washauriwa kutumia maabara ya DIT

A7b0d419f12a9a20929e8151d52b74b7.jpeg Wakulima wa embe washauriwa kutumia maabara ya DIT

Mon, 20 Dec 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Wakulima wa matunda hususan zao la embe wameshauriwa kutumia maabara ya kupima udongo ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) ili kuwa na uhakika wa aina ya udongo uliopo kwenye shamba husika ili aweze kuchukua hatua stahiki kuwezesha tija Mikoa inayohusika ni ya Dar es Salaam, Pwani, Arusha na Kilimanjaro.

Naibu Mkuu wa Taasisi, Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu kutoka taasisi hiyo, Profesa Patrick Nsimama alisema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja yaliyoratibiwa na DIT kupitia Mradi wa Utafiti wa masuala ya Kilimo ujulikanao kama ADEMNIA.

Alisema kwa kutumia maabara hiyo zao la embe litaongezeka kwa kuwa wakulima watashauriwa eneo linalofaa la kilimo hicho. Mratibu wa Mradi huo Dk Joseph Matiko alisema Mradi huo wa miaka mitano unafadhiliwa na Serikali ya Norway na una lengo la kuboresha huduma za kilimo kwa kupambana na wadudu waharibifu wa mazao.

Naye Hamadi Mkopi alizungumzia kuhusu udhibiti wa inzi wa embe na utunzaji wa zao hilo baada ya kuvunwa kwa kusema wadudu wanaosumbua katika kilimo cha matunda ni wengi ila katika zao la embe mdudu hatarishi ni inzi.

Alisema inzi huyo huharibu kati ya asilimia 50 hadi 80 ya zao la embe hivyo juhudi za kumdhibiti kwa kutumia mitego ya asili zimeonyesha mafanikio. Mafunzo hayo ni ya utunzaji wa zao la embe kwa wakulima wa zao hilo iliyofanyika katika shamba la maembe la KOGA lililopo Mkuranga Mkoani Pwani linalomilikiwa na mkulima Dk Salim Diwani.

Chanzo: www.habarileo.co.tz