Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima wa Mtama Dodoma kuondokana na umasikini

Patrick Mbeho.jpeg Mkulima wa Mtama, Patrick Mbeho akiwa ni mmoja wa wanufaika wa mpango wa WFP na FARMAFRICA

Wed, 2 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MRADI wa Kilimo Himilivu cha Mtama(CSA) kinachosomamiwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani ( WFP)umekuwa chachu ya maendeleo kwa wakulima wa zao hilo kwenye Wilaya sita za Mkoa wa Dodoma.

Kwa mujibu wa WFP ni kwamba kupitia mradi huo wakulima hao wanevuna na kuuza mtama tani 28000 wenye thamani ya Sh.bilioni 13 5 kwa msimu wa Kilimo wa mwaka 2020/2021.

Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma ,Mkuu wa Ofisi Ndogo ya WFP Neema Sitta amesema mradi huo umeleta tija kubwa kwa wakulima ambao kwa Sasa mbali ya kuvuna mtama mwingi pia wamekuwa na soko la uhakika ,hivyo hakuna changamoto ya kukosa soko kwani lipo la uhakika.

"Mradi wa CSA unatekelezwa katika vijjji zaidi ya 200 vilivyopo kwenye wilaya sita za Mpwapwa,Chamwino, Bahi, Kongwa, Chemba na Kondoa ambapo kwa msimu wa mwaka 2020 hadi 2021 wamefanikiwa kuuza zaidi ya tani 28,000 za mtama, zenye thamani ya Sh. bilioni 13.5.

"Wanaofadhili mradi huu ni Shirika la Maendeleo ya Ireland (IrishAid) na kusimamiwa na WFP lakini wanaoutekeleza ni FarmAfrica kwa Sh.bilioni 1.7.Uzuri wa mradi huu umegusa wakulima 22,000 na kunufaisha zaidi ya watu 100,000,"amesema.

Aidha Sitta amesema matarajio yao ni kuona wakulima wa mtama wanaongeza uzalishaji katika msimu huu mpya wa kilimo na WFP wako tayari katika kuhakikisha wanashirikiana kikamilifu na wakulima hao wa mtama.Sababu ya kuamua kujikita katika kilimo cha mtama ni kutokana na zao hilo kukubali kwenye ardhi na mazingira ya Dodoma, pamoja na uhakika wa soko".

Amefafanua soko kubwa la zao la Mtama kwa hapa nchini linahusisha wanunuzi wakubwa na miongoni mwao ni Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) na kampuni nyingine za ndani na nje ya nchi.Pia kuna soko la Mtama mweupe Sudani Kusini.

"WFP na FarmAfrika kupitia nradi wa kilimo himilivu tumeweza kuunganisha wakulima na kubwa zaidi kuwa na soko la uhakika na kwa sasa bei ya zao la mtama kilo moja inaunzwa Sh.550 kutoka Sh. 250 ya awali ,"amesema.

Kwa upande wa Meneja Mradi wa Kilimo Himilivu cha Mtama kutoka Shirika la FarmAfrica Tanzania Grace Changanyika amefafanua kupitia mradi huo wakulima wa mtama wamepiga hatua kubwa ya kimaendeleo.

Wakati huo huo baadhi ya wakulima wa zao hilo wameishukuru WFP na FarmAfrica kwa kuwapelekea mradi huo ambao umewawezesha hivi kuwa na tofauti kubwa katika maisha."Kwa sasa hata vipato vyetu, tunavuna mtama kwa wingi tofauti na hapo nyuma kabla ya kuja kwa mradi huu."

Mmoja ya wakulima wa zao la Mtama ambao wananufaika na mradi huo akiwemo Patrick Mbeho ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Mkola wilayani Bahi amesema mradi huo umefanya mapinduzi makubwa kwenye maisha yake,amekuwa na mafanikio makubwa.

“Kwangu haya ni mapinduzi ya kiuchumi, kijamii na maendeleo kwani nilikuwa napata Sh. milioni mbili kwa shamba la hekari 20 ila kwa sasa napata hadi Sh. milioni sita na wakati mwingine Sh.milioni Saba.Nimejenga nyumba ya biashara,pia ninayo mashine ya kupembulia mtama na mengine mengi,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live