Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima pamba walia ubovu mizani

Wadau Wakulima pamba walia ubovu mizani

Thu, 27 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Wakulima wamepaza kilio hicho kwenye kikao cha wadau wa pamba mkoani Shinyanga, kilichokuwa na lengo la kujadili changamoto za zao hilo, hasa kuelekea kwenye ununuzi wake.

Mmoja wa wakulima hao wa Pamba, Raphael Sospeter, ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha msingi cha ushirika (Amcos) ya Gimagi wilayani Kishapu, alisema mizani mingi ambayo inatumiwa kununua Pamba ni mibovu inapunja kilo.

"Mizani ambayo inatumika kununua pamba kutoka kwa mkulima kupitia Amcos, ambayo hutolewa na chama kikuu cha ushirika mkoani Shinyanga (SHIRECU) imesha zeeka ina punja sana kilo, hivyo tunaomba itumike mizani ya kwenye makampuni,"alisema Sospeter.

Naye Kaimu mrajisi wa vyama vya ushirika mkoani Shinyanga, Hilda Boniphace, alisema ni kweli mizani inayotumika kwenye Amcos kununua Pamba ya Mkulima imeshachoka, na kubainisha hata kama ikifanyiwa matengenezo haiwezi kutengemaa, na ana taarifa ya mizani 20 ambayo ni mibovu kabisa.

Aidha kaimu meneja wakala wa vipimo mkoani Shinyanga, Hilolimus Mahundi, alisema mizani siyo mingi mibovu, isipokuwa inachezewa, pamoja na ile ya Digital kuishiwa nguvu ya umeme.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dk. Philemon Sengati, alisema suala hilo la ubovu wa mizani liangaliwe, ili mkulima asipunjwe kilo na pamba yake ipate kumnufaisha na kuinuka kiuchumi.

Pia alisema katika msimu wa kilimo (2020/2021) wakulima waliolima Pamba ni 39,923, eneo lililolimwa ni Hekta 82,180, na Matarajio ni kuvunwa Tani 51,363.

Chanzo: ippmedia.com