Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakulima mtama kunufaika na fursa

MTAMA Wakulima mtama kunufaika na fursa

Sat, 25 Apr 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KITUO cha utafiti za mbegu bora za kilimo TARI Hombolo jijini Dodoma, kimeingia mkataba wenye thamani ya dola za kimarekani 11,000 na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa ajili ya kutafiti na kuzalisha mtama unaotakiwa katika kutengeneza bia.

Mkataba huo umefadhiliwa na Shirika la Afrika Kusini la AB INBEV.??Dk. Lammeck Makoe, ambaye ni mtafiti Mkuu wa TARI Hombolo Bwawani, alisema mkataba huo utasaidia kwa kiasi kikubwa sana katika kuzalisha mtama huo ambao unahitajia kwa ajili ya kuazalisha bia nchini.??

Dk. Makoe alisema wao kama TARI wamefurahi kupata mkataba huo, huku akiwataka Watanzania kujiandaa kunufaika kwa fursa hiyo kutokana nchi kuwa na mbegu za mtama zilizo bora ambazo zitakuwa na soko kwa ajili ya kutengeneza bia.

??“Tumefurahi kupata mkataba huo kwa sababu tunaamini utasaidia sana wakulima wa mtama kupata mbegu bora za mtama,” alisema Dk. Makoe.??

Alisema kilio cha wakulima ni kuhakikisha wanapata mbegu bora, hivyo mkataba huo ni neema kwao kwa sababu wana uhakika wa kuzalisha mbegu ambazo zinahitajika katika kuzalisha mtama huo unaohitajika kutengeneza bia.??

Hata hivyo, alisema wakulima wanapaswa kuchangamkia fursa pale tu watakapoona mbegu hizo zimeanza kutolewa kwaajili ya watu kuanza kupanda mtama huo unaotakiwa kwa ajili ya bia.

Hata hivyo, alisema wakulima wanapaswa kuchangamkia fursa pale tu watakapoona mbegu hizo zimeanza kutolewa kwaajili ya watu kuanza kupanda mtama huo unaotakiwa kwa ajili ya bia.

??Alifafanua zaidi kuwa, hivi sasa wakulima wa mtama watakuwa na uhakika kuwa wakilima mtama huo watakuwa na mahali pa kuuzia kutokana na TBL kuwa pamoja nao katika uzalishaji wa bia.??

Naye Mkulima wa zao hilo, Juma Lubeleje, alisema wamekuwa wakihangaika na soko la mtama, lakini hivi sasa wanaamini soko lao litakuwa kwa sababu mahali pa kuuza kupo.??

Alisema wanaishukuru TBL kwa kuonyesha njia baada ya kuingia mkataba huo na shirika hilo pamoja na TARI ambapo wanaamini watakuwa wakombozi wa wakulima katika eneo hilo.??

“Tumefurahi sana kupata neema hii, tutajitahidi kulima kwa wingi ili?tuweze kuuza mtama ambao utatusaidia katika kuongeza kipato na familia zetu,”alisema Lebeleje.??

Alisema yeye na wakulima wenzake wanasubiri tu mbegu hizo zitoke ili waanze kuzitumia katika kupanda na baadae wakati wa mavuno watakuwa na uhakika wa soko la mtama ambao unahitajika kutengeneza bia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live